Kuna mhusika mmoja kwenye series ya The Undoing alisema jambo lililonifanya niandike hii makala.

Walikuwa kina mama kadhaa wakimteta mwanamama mwenzao aliyejiunga hivi karibuni kwenye kikundi chao kinchojihusisha na  maswala ya fundraising pamoja na mambo mengine.

Kwa ufupi stori ilikuwa hivi; huyu mwanamama mgeni alikuwa yupo yupo tu. Alionekana kama hafanyi kazi yoyote. Wenzake walimshangaa unawezaje kuishi katikati ya jiji la New York, Manhattan halafu ukawa upo upo tu, haujishughulishi. New York ni mji wa mishe mishe na mikiki mikiki, siyo wa kukaa kizembe. 

Basi katika kumteta mwanamama huyu, mhusika mmoja akasema na ninamnukuu; ‘I feel like telling her, “You live in New York. It is a crime not to be frantically busy”. Akiwa na maana kwamba ni jambo la ajabu mtu kukaa katika jiji la New York halafu haujishughulishi.

The Undoing, HBO

Kauli hiyo ya ‘It is a crime not to be frantically busy in New York’ ilinifikirisha kidogo na ndiyo imenifanya niandike makala haya.

Jinsi ya Kuwa Mbele Ya Muda Kiujuzi na Maarifa ya Kazi

Ukitaka kuwa mbele ya muda KIUJUZI na MAARIFA ya Kazi, usiangalie tu soko la ajira la hapa Tanzania. We’re still struggling with digitization and digital transformation here.

Bali jaribu kuangalia kama skills ulizonazo zinakuwesha kupata kazi pale Silicon Valley au Wall Street (yes, shoot for the goddamn moon). 

Jiulize soko la ajira katika miji iliyoendelea kama Hong Kong au New York linahitaji ujuzi na maarifa ya aina gani? What does it mean to be a professional there? What does it take to not only survive but thrive in those places?

Ukiweza kuwa competitive kwenye job market ya huko, believe me utakuwa more than five years ahead the local market. Na wewe utakuwa hautafuti kazi tena bali kazi zinakutafuta!

Maendeleo ya kidigitali, teknolojia, na kazi kwa ujumla tutakayoyapata hapa Tanzania in the next five years, tayari yamefikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye miji iliyoendelea. Jaribu kujipima kwenye mizani hiyo. 

Sababu nyingine kwanini usiangalie soko la hapa nyumbani tu ni hii 👉🏽 katika dunia ya remote working, mtu aliyeko india anatafuta kazi popote duniani ikiwemo tanzania. Mtu wa kenya vile vile. Sasa kwanini wewe Mtanzania ung’ang’anie soko la hapa nyumbani tu?

Share makala hii kwa mdau mwingine ili naye aanze kujitazama katika mizani tofauti ya ujuzi na maarifa ya kazi.